Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuwa wizara hiyo kwa ushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mkioa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) zinatarajia kuendesha kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya ugpnjwa wa polio kwa watoto zaidi ya milioni tatu nchini walio chini na umri wa miaka 8.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Ummy amesema watoto watakaopatiwa chanjo hiyo ni wa mikoa sita ambayo ni Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na Mbeya.

Amesema maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa polio yametolewa taarifa pia katika nchi zinazopakana na Tanzania.

Tanzania inaendesha kampeni hiyo ya chanjo kutokana na wizara ya afya kupokea taarifa Mei 26,2023 za uwepo wa mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka na miezi sita au saba na miezi kumi na moja ambaye alionesha dalili za kupooza kwa ghafla katika manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Uchunguzi wa maabara ulithibitisha kuwa mtoto huyo ana maambukizi ya virusi cha Polio.

Written by Janeth Jovin

Photo of Yasini Ngitu