EXCLUSIVE: Mbunge Mteule Jimbo la Tundu Lissu, Afunguka Mazito! – Video

MBUNGE Mteule wa Jimbo la Singida Mashariki, lililokuwa likiwakilishwa na,  Tundu Lissu, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Miraji  Mtaturu, amedai kuwa Tundu Lissu hajawahi kuzungumzia maendeleo ya maji wala barabara katika jimbo hilo kwa kipindi cha miaka tisa ya ubunge wake.

Mbunge huyo amejitambulisha kuwa amezaliwa miaka 49 iliyopita na amekuwa katika utumishi wa aina mbalimbali katika mashirika ya umma, nafasi ya mtendaji wa CCM,  ukatibu wa wilaya,  mkuu wa wa wilaya ya Ikungi  na Katibu wa CCM  Mkoa wa Mwanza mwaka 2015.

Ameeleza zaidi kwamba alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Igungi toka 2016 mpaka leo 2019 kabla ya kuwa mbunge mteule na kwamba atafanya juu-chini kushirikiana na mkuu wa wilaya hiyo na kuisimamia serikali kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.


Toa comment