Viongozi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Vya TGNP Walivyoibua Changamoto
Afisa Habari wa TGNP, Monica John akizungumza na wanasemina.
Viongozi wa vituo vya Taarifa na Maarifa vilivyopo chini ya Mtandao wa Jinsia (TGNP) wameendelea kujibua changamoto kwenye kata zao mbele ya wanahabari walioshiriki nao semina ya pamoja.
Semina hiyo ya siku mbili ilifanyika Machi 26 na Machi 27 ilifanyika Makao Makuu ya Mtandao huo Mabibo Dar ambapo viongozi wa vituo hivyo katika Kata za Saranga, Mabwepande, Majohe na Kivule walikuwa wakielezea changamoto walizoziibua.
Viongozi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Saranga wakifuatilia kiumakini semina hiyo.
Miongoni mwa changamoto hizo ilikuwa ni upande wa miundombinu, ikiwemo ubovu wa barabara, ukosefu wa madaraja, ambapo suala la elimu nalo liliibuliwa changamoto mbalimbali.
Upande wa elimu viongozi wa kata ya Kivule waliibua changamoto kwenye Shule ya Msingi Kivule Annex yenye wanafunzi 684 na kubaini kuwa haina choo hata kimoja.
Mwanahabari Daniel Semberya akichangia mada kwenye semina hiyo.
Viongozi wa Kata ya Mabwepande nao walielezea changamoto mbalimbali zilizopo kwenye zao ambapo pia walielezea na changamoto iliyopo Sekondari ya Mabwepande hali iliyopelekea shule hiyo kushika mkia katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana.
Viongozi hao walisema katika shule hiyo kwanza kuna uhaba wa walimu jambo linasababisha ufundishaji uwe duni.
Viongozi wa Kivule, Erick Anderson (kushoto) na Sarah Mharagi wakieleza changamotoa walizoziibua kwenye kata yao.
Wakiendelea kuibua changamoto hizo walisema shule hiyo haina uzio jambo linalosababisha wahuni kuingia maeneo ya shule hiyo na kusumbua wanafunzi.
Wamesema pia ukosefu wa uzio unasababisha wanafunzi kupata mwanya wa kutoroka na kuacha masomo.
Mratibu wa Miradi (TGNP) Anna Sangai naye akitoa somo kwenye semina hiyo. Upande wa barabara viongozi wa Mabwepande waliizungumzia ubovu wa barabara yao inayoanzia Bunju B kuelekea Mabwepande ambayo imeharibika mpaka daladala zilizokuwa zikifanya ‘ruti’ ya Makumbusho mpaka Mabwepande kuishia Bunju B kufuatia ubovu wa barabara hiyo na hivyo kuwalazimu kukodi Bajaj au Pikipiki ili kufika Mabwepande.
Kiongozi wa Kituo cha Mabwepande, Costansia (kulia) akielezea changamoto walizoziibua kwenye kata hiyo, katikati ni Fatuma Murr na kushoto ni Jamila Hamisi nao wakisubiri kuwasilisha changamoto hizo. Baada ya viongozi wa kata zote nne zilizoshiriki semina hiyo na kuibua changamoto hizo wanahabari hao walipeana majukumu ya kuzifuatilia na kuziweka hadharani ili viongozi wanaohusika wachukue hatua.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS GPL
