Yanga Yaipiga Moro Kids Bao 2-0, Juma Balinya Atupia

Kikosi kipya cha timu ya Yanga kilichocheza  ya dhidi ya Moro Kids.

YANGA imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kirafiki, baada ya jana asubuhi kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Moro Kids.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Highland uliopo Chuo cha Biblia maeneo ya Bigwa, mabao ya Yanga yalifungwa kipindi cha kwanza na Juma Balinya kwa njia ya penalti baada ya Issa Bigirimana kuchezewa rafu.

Bao la pili lilifungwa na Paulo Godfrey ‘Boxer’ baada ya kuwatoka mabeki wa Moro Kids, na kufanikiwa kupiga shuti kali lililojaa wavuni. Katika mchezo huo, kipa Klaus Kindoki aliumia baada ya kugongana na mshambuliaji wa Moro Kids, hali iliyosababisha kuondolewa uwanjani kwa kubebwa na beki, Lamine Moro,  na nafasi yake ikachukuliwa na Metacha Mnata.

Juma Balinya akifanya yake.


Toa comment